Monday, January 2, 2012

NDOTO ZISIZO TAFSILIKA

52.NDOTO ZISIZOFASIRIWA.

Kuna baadhi ya ndoto huwa haziwezekani kufasiriwa kutokana na jinsi hali ya mtu wakati alipoota au kufuatana na ndoto jinsi ilivyootwa. Nazo ni kama zifuatazo:

1. Wakati mtu kalala hali ana janaba.
2. Wakati mtu kalala hali kalewa.
3. Mtu kabla ya kulala akawa anafikiri kitu na kukitamani kitu kile kisha akaota vilevile.
4. Ndoto mbaya yenye kukhofisha na kuhuzunisha ya kutokana na Shetani.

121.FAIDA ZA NDOTO.
Baada ya utafiti katika kujua ndoto nimekuja kufahamu kwamba Mwenyezi Mungu S.W.T. ametukirimu sisi binadamu na hasa Waislamu wema kwa kuota ndoto za kweli kwa kuwabashiria ambazo ndoto hizo zina faida kama ifuatavyo:

1. Ni njia mojawapo ya kuwaona na kujua hali za maiti ambao khabari zao zimetukatikia walipoihama dunia. Kama alivyotuhadithia Sahaba Ibn Abbas R.A.A. kwamba roho za wale watu waliokufa zinakutana na roho za walio hai na kuulizana baina yao. Pia huenda tukafahamu hali ya yule maiti ima katika raha au taabu. Mtu Fulani alinielezea kwamba alimuota ndugu yake katika ndoto. Yule ndugu yake aliyekufa akamwambia kwamba mimi niko katika hiki chumba siwezi kulala. Na yule maiti alipokuwa mzima duniani alikuwa hasali. Kwa hiyo ndugu yake alijua hali ya yule maiti wao jinsi alivyo. Na mfano mwingine kuna mwanamke Fulani alikufa baada ya kifo chake watu wakawa wanasema kwamba karogwa. Mmoja wa ndugu yake alimuota ndotoni kama vile yuko katika bustani lenye maua mazuri yenye rangi mbalimbali. Na yule mwanamke alikuwa amekaa kwenye kizingiti cha nyumba na amebadilika kawa msichana mzuri, mara tu yule ndugu yake alipojitokeza mwanamke yule akamsalimia kwa kusema, "Assalaamu Alaykum" kisha akenda zake wala hakumuona. Kwa hivyo ndugu zake walijua hali ya maiti wao.

2. Ni njia moja ya mja kutishwa na kuogopeshwa na Mola wake kwa sababu ya dhambi/madhambi aliyofanya ili ajirekebishe tabiya yake. Mtu Fulani alinielezea kuhusu ndoto aliyoiota ya kutisha usingizini mwake. Mimi nikamwambia kwamba huenda umefanya kitendo kibaya na Mwenyezi Mungu S.W.T. anataka kukuongoza ili usiendelee kufanya kitendo hicho tena. Halafu akasema kwamba ni kweli nimekwisha tambua kosa langu. Na kosa lake lilikuwa kamtolea maneno mabaya mfanyakazi wake wa kike.

3. Ni njia ambayo inatujulisha hali ya watu wanaotuhusu waliohai lakini wako mbali nasi katika hii dunia. Kama alivyotusimulia Mtume S.A.W. kwamba hakika roho hukutana na roho nyingine. Mfano mtu anaishi Oman akamuota ndugu yake ambaye yuko huko Tanzania ambapo hawakuonana naye kwa miaka. Labda huenda akamwambia jambo fulani la siri au akajua hali yake alivyo, mfano mgonjwa.

4. Ni njia ya kusemeshana baina ya maiti na aliyehai. Mfano baba aliyekufa na kuacha deni humwambia mwanawe ndotoni kwamba mimi na deni fulani na ananidai mtu Fulani kwa hiyo tafadhali nilipie hilo deni. Na ajabu kubwa anapouliza hutokea kweli kama alivyoambiwa na baba yake ndotoni.

5. Ni njia ya kumuongoza mja katika haki na kujiepusha na baatil. Mfano mwanamke Fulani alinilielezea kisa ambacho ameota ndotoni kama ifuatavyo: Ameota kama kwamba anaoneshwa Mtume S.A.W. lakini yeye hamuoni. Baadaye kama mtu akamwambia ndotoni kwamba ukitaka kumuona basi lazima uache mambo mabaya unayoyafanya. Baada ya kumhoji ikatokea kweli kwamba yeye anapenda kusikiliza miziki na kufanya mambo ambayo yamekatazwa katika sheria ya dini.

6. Ni njia ya Mola kumuonesha mja katika ndoto amali njema/mbaya anayoifanya.


Asalam Alaikum Waarahmatullahi Wabarakatuhu MIMI NI KIJANA NA




NDOTO YA MSICHANA AMEOTA MCHUMBA WAKE AMEKUJA KUMCHUKUWA KWA GARI.

Msichana Fulani ameota anasema: Mimi nimeota kuwa mchumba wangu aliyekuwa nje ya nchi amekuja kunichukuwa kwa gari yake. Tukavuka daraja kwa gari na pembezoni mwa ile barabara yote ilikuwa imepandwa miti pamoja na miwaridi. Baadaye tukafika katika nyumba fulani ambayo nyumba hiyo ilikuwa na milango miwili. Yeye aliingia katika mlango mkubwa nami niliingia katika mlango mdogo ambao ulikuwa umefungwa kisha nikaufungua. Na nilipoingia ndani niliona pia miti katika bustani ya nyumba halafu nikamuona mchumba wangu ameingia kuoga, alipotoka akaanza kuvaa nguo nzuri kabisa na kuliani kwake msahafu na amefuatwa na kijana mdogo kuliko yeye kwa umri. Baada ya hapo akaniambia, "Haya tutoke nje." Nikatoka pamoja naye. Jee, nini tafsiri yake?


Mfasiri akamwambia: Ndoto yako ni khabari njema kwa ubora wa kuchagua kwako mume mwema. Kisha amejisafisha na madhambi na msahafu kuliani kwake. Ama vazi lake katika nguo nzuri ni wewe. Kwani vazi la mume ni mke wake.


NDOTO YA MWANAMKE AMEOTA AMEPEWA MAYAI MATATU.

Mwanamke Fulani ameota anasema: Mimi nimeota mjomba wangu amenipa mayai matatu nikayapokea kwa mikono miwili. Jee, nini tafsiri yake?


Mfasiri akamwambia: Ndoto inaashiria kwamba utazaa mabinti watatu baada ya kufunga ndoa.
NDOTO YA MWANAMKE AMEOTA KATIKA NYUMBA YAO PANYA WENGI PAMOJA NA NYUKI WENGI

Mwanamke Fulani ameota anasema: Mimi nimeota katika nyumba yetu panya wengi wanaingia jikoni kisha wanatoka, halafu wanakwenda chumba kingine. Kisha mimi na mume wangu pamoja na wanangu tukaanza kusafisha nyumba kwa detol, baadaye kama tukatoka nje ya nyumba. Tena niliporejea nikaona nyuki wengi wameingia nyumbani lakini sikuwakuta panya. Na nyuki mmoja akaniuma mguuni. Naomba tafsiri yake.



Mfasiri akamwambia: Nyinyi mlikuwa mna kazi inayowaletea rizki lakini mliipuuza na kuiacha. Mkashika kazi mpya hata hivyo pia inawaleteeni faida. Lakini wewe utapatwa na udhia kutoka kwa watu watakaojiingiza katika shughuli hiyo.

NDOTO YA MTU AMEOTA MENDE WENGI JUU YA PAA LA NYUMBA YAO.
Mtu mmoja ameota anasema: Mimi nimeota ndotoni mende wengi juu ya paa la nyumba yetu. Kisha nikaleta dawa ya kupuliza, nikawapulizia baadaye hakubakia hata mende mmoja juu ya paa ila wote walikimbia na kujificha. Lakini nilimkuta mende mmoja tu yupo juu ya heater la kuchemshia maji.


Mfasiri akamwambia: Mwenyezi Mungu anajua, nyumba yenu ina kitu kinachotokana na hasad, lakini Mola atakiondosha insha-allah.

NDOTO YA MWANAMKE AMEOTA ANASHAMBULIWA NA PANYA WENGI.
Mwanamke Fulani ameota anasema: Mimi nimeota niko katika nyumba ngeni ambayo sijapata kuiona katika maisha yangu. Mara wakaja panya wengi wenye rangi ya kijivu wakanishambulia wakaanza kuutafuna mkono wangu wa kulia na huku mimi nautikisa na kuuyumbisha. Lakini wapi! Wale panya wameung`anga`nia hawataki kuuachia. Na mimi sikujua nini la kufanya, baadaye nikasoma Ayatul Kursiy kwa sauti kubwa nikaendelea hivyo mpaka wale panya wakaanza kuuachia. Lakini kitu cha kushangaza ni kwamba mkono wangu ulikuwa unaniuma wakati wale panya wako mkononi, walipokimbia mkono ukarejea kama kawaida wala sikuhisi kitu. Nikawa natafuta hospitali ili niende wakauone ingawa mimi sikuhisi kitu chochote.




Mfasiri akamwambia: Mwenyezi Mungu anajua, kama inavyodhihirika ndoto yako wewe unakesha wakati mwingine, inakuwa usiku wako ni mchana na mchana wako ni usiku. Lakini hutadhurika Inshaa-allah. Na panya kuutafuna mkono wako wa kulia hiyo itaathiri riziki yako. Ni juu yako kwenda mapema kulala hata upate riziki.




NDOTO YA MWANAMKE AMEOTA ANAZAA SAMAKI WENGI KISHA WAKAGEUKA NYOKA WENGI WADOGO.
Mwanamke mmoja anaelezea ndoto yake anasema: Mimi nimeota nazaa na mzalishaji alikuwa pamoja na mimi ananisaidia wakati wote ule wa kuzaa. Nilikuwa nikihisi maumivu makali sana. Nikazaa samaki wengi baadaye hao samaki wageuka nakuwa nyoka wengi wadogo. Na ilikuwa ikinitoka vipande vya damu wakati wa kuzaa. Kisha nikaamka na ilikuwa wakati huo wa Alfajiri. Jee, nini tafsiri ya ndoto hii.


Mfasiri akamwambia: Kuzaa ni raha, kupata faraji, kulipa madeni na toba. Na samaki ni mali. Wewe unapenda uruzukiwe. Lakini hiyo mali itakayopatikana ni katika njia mbaya. Kwasababu samaki wamegeuka kuwa nyoka. Na mapande ya damu katika ndoto ni mali isiyo ya halali au dhambi. Lakini wewe utakapojua utatubia kwa msaada wa watu. Na maumivu ndotoni ni kujuta kwa dhambi.


5.NDOTO YA MTU AMEOTA NYUMBA YAKE IMEJAA NYOKA WENGI.

Mtu Fulani alimjia Ibn Siyriin akamhadithia ndoto yake akasema: Mimi nimeota nyumba yangu imejaa nyoka wengi.


Akamfasiria akamwambia: Mche-Mungu usiwaweke nyumbani kwako maadui wa Waislamu.

DOTO YA MWANAMKE AMEOTA AMEKWENDA KWA SHOGA YA MAMA YAKE AKAKATWA NYWELE ZAKE.
Mwanamke mmoja ameota anasema: Mimi nimeota ndotoni nimekwenda kwa shoga ya mama yangu, na mahali hapo anapoishi pana sehemu ya kunyolea. Naye ndiye alikuwa kinyozi akanikata nywele zangu. Lakini kusema kweli yeye si kinyozi. Baada ya kunikata mimi sikupendezewa na mkato wa nywele zangu zilivyokatwa. Jee, nini tafsiri yake?


Mfasiri akamwambia: Ndoto inaashiria patatokea ugomvi baina yako na baina ya mtu wa karibu yako kwasababu ya mwanamke fulani anakufanyia ubaya. Na wewe pia unabeba sehemu ya jukumu kwa ugomvi utakaotokea.


NDOTO YA MWANAMKE ALIYEOLEWA AMEOTA ANAAMBIWA NA BABA YAKE, "ATAOLEWA NA MUME WAKE."
Mwanamke Fulani anasema: Dada yangu aliyeolewa ameota ameachwa. Akamjia baba yangu na fustani ya harusi akamwambia, "Leo ni ndoa yako atakuoa mume wako." Akaichukua ile fustani akampa dada yake mkubwa (hajaolewa) akamwambia, "Wewe olewa nayo hii fustani." Akaichukua dada yangu mkubwa ile fustani na alikuwa nacho kikuku (aina ya bangili) cheupe akampa dada yangu mdogo kwa mkufu mwingine kutoka kwa mume wa dada yangu akamwambia, "Hii ni nzuri kuliko aliyonayo mkononi dada yangu mkubwa" Dada yangu mdogo akenda nayo ile fustani na mkufu kwa dada aliyeolewa kusudi ajaribu kumridhisha ili olewe. Akazichukua akenda nazo kwa baba yangu. Nilikuwa mimi na yeye na baba yangu, akazungumza baba yangu kwamba leo ni ndoa yangu mimi na yeye. Nilikuwa nayo fustani nyeupe pia. Baba yangu akasema, "Dada yako ataolewa na mfanyabiashara tajiri na atakuwa mwenye furaha." Akasimama na huku amekasirika kwasababu ya maisha yake. Baba yangu akamwambia, "Usikasirike na ndoa yako hii, ni bora kuliko ya mwanzo." Akamjibu, "Ndoa ya mwanzo ilikuwa jeneza na kuingia nyumba ya mume wangu ni kaburi." Baba yangu akamjibu, "Ndoa yako hii ni afadhali kuliko ndoa iliyopita." Kwahiyo akaridhika. Jee, nini tafsiri yake?



Mfasiri akamwambia: Mwenyezi Mungu anajua, pengine ndoto yake inaashiria posa itakayokubalika kutoka kwa mwanaume mwingine si huyo mtalaka wake. Na huyo mwanaume ni mwenye mali na mwenye tabia nzuri. Na mkufu ni kufunga ndoa na fustani nyeupe ni furaha njema sana.

NDOTO YA MWANAMKE AMEOTA WATU WANAMWITA BINTI YAKE HURULAENI.

Mwanamke mmoja ameota anasema: Mimi nimeota jina la binti yangu limebadilika, watu wanamwita kwa jina la, "Hurulaeni." Ila mimi tu namwita kwa jina lake. Jee, nini tafsiri yake? Ifahamike kwamba mimi ninaye huyu binti mmoja tu.


Mfasiri akamwambia: Mwenyezi Mungu anajua, pengine binti yako ni mzuri sana wa kupendeza mwenye macho makubwa na yaliyopakwa wanja. Anavutia na macho ya watu yanamuelekea yeye. Kwahiyo ni juu yenu kumwepusha na kijicho cha watu na hasad.
NDOTO YA MWANAMKE AMEOTA YUPO PAMOJA NA MAKASISI NA WATAWA WA KIKE NDANI YA GARI.
Mwanamke Fulani ameota anasema: Mimi ni Mwanamke Mwislamu ambaye nimeolewa, lakini nimeota niko ndani ya gari tunaelekea kanisani nikiwa pamoja na makasisi (priests) na watawa wa kike (nuns). Na tulipowasili tuliingia wote pamoja kanisani. Jee, nini tafsiri yake?


Mfasiri akamwambia: Mwenyezi Mungu anajua, wewe unahudhuria hafla (sherehe) za harusi zina baadhi ya nyimbo na kucheza ngoma.

NDOTO YA MWANAMKE AMEOTA YUPO PAMOJA NA MAKASISI NA WATAWA WA KIKE NDANI YA GARI.
Mwanamke Fulani ameota anasema: Mimi ni Mwanamke Mwislamu ambaye nimeolewa, lakini nimeota niko ndani ya gari tunaelekea kanisani nikiwa pamoja na makasisi (priests) na watawa wa kike (nuns). Na tulipowasili tuliingia wote pamoja kanisani. Jee, nini tafsiri yake?


Mfasiri akamwambia: Mwenyezi Mungu anajua, wewe unahudhuria hafla (sherehe) za harusi zina baadhi ya nyimbo na kucheza ngoma.

265.NDOTO YA MWANAMKE ALIYEOLEWA AMEOTWA ANAOLEWA MARA YA PILI.
Mwanamke mmoja ameotwa anasema: Mimi ni mwanamke niliyeolewa na nina watoto wawili wala sifanyi kazi. Dada yangu ameniota naye ni mdogo kwangu kwamba nimevaa fustani (gauni) ya harusi nzuri sana bila ya veli ya harusi. Nami nimekaa katika nyumba ya familia yangu. Na watu na majirani wamekusanyika kama vile sherehe ya harusi, na mume wangu na watoto wangu wamehudhuria pia. Dada yangu alikuwa akishangaa vipi naolewa mara ya pili, nami nimekwisha olewa na mume wangu na watoto wangu wamehudhuria sherehe ya harusi? Naomba tafsiri ya hii ndoto.


Mfasiri akamwambia: Utapata furaha mfano wa furaha ya ndoa, ya kazi nzuri, au mimba au kukubaliwa kusoma Chuo Kikuu.

NDOTO YA MWANAMKE AMEOTA YUPO HOSPITALINI.
Mwanamke mmoja ameota anaelezea anasema: Mimi nimeota niko hospitalini lakini hakunizuru mtu yeyote yule katika jamaa zangu na hata tabibu, na hospitali hiyo inaitwa Sa`ad. Na katika kitanda changu palikuwa na msichana pamoja na jamaa yake akanisalimia kisha akanibusu wakaondoka wote nikabaki peke yangu. Kisha nikajiona nimesimama katika mlango wa ukumbi na katika mkono wangu wa kushoto Qur-ani na karatasi yake ina rangi nyekundu. Lakini maandishi yake ni ya rangi nyeusi. Na mtoto wa kiume wa mama yangu mdogo alikuwa akiisoma halafu akaondoka. Na mimi nikaingia katika ukumbi nikakaa hapo.


Mfasiri akamwambia: Ndoto yako ya hospitali inayoitwa Sa`ad ni dalili kwamba wewe unangojea muradi (jambo/haja inayohitajiwa kupatikana). Wapo wasichana wa jamaa zako waliokaribu wataolewa kabla yako. Lakini hata wewe pia ni karibu. Na kusoma Qur-ani ni dalili ya mtoto wa mama yako mdogo anarejesha amana za watu na ameongoka katika haki. Anaamrisha mema na anakataza maovu kwa kauli ya Mola (...Wanasoma Aya za Mwenyezi Mungu nyakati za usiku, na pia wanasujudu. Wanamuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, na wanaamrisha mema na wanakataza maovu...)

NDOTO YA MWANAMKE AMBAYE HAJAOLEWA AMEOTA AMEZAA MTOTO WA KIKE.

Mwanamke mmoja ameota anasema: Mimi ni mwanamke sijaolewa nimeota nimezaa mtoto wa kike. Jee, nini tafsiri yake?




Mfasiri akamwambia: Ndoto ya wewe kuzaa mtoto wa kike ni dunia na mlango wa kheri na furaha.


NDOTO YA MWANAMKE MJAMZITO AMEOTA AMEZAA MTOTO MZURI.
Mwanamke Fulani ameota anasema: Mimi ni mwanamke mjamzito nimeota nimezaa mtoto mweupe mzuri. Jee, nini tafsiri yake?



Mfasiri akamwambia: Ndoto inaashiria kwamba kweli utazaa mtoto mzuri. Lakini jihadhari naye asije akapigwa kijicho.
NDOTO YA MWANAMKE MJAMZITO AMEOTA AMEZAA MTOTO MZURI.

Mwanamke Fulani ameota anasema: Mimi ni mwanamke mjamzito nimeota nimezaa mtoto mweupe mzuri. Jee, nini tafsiri yake?



Mfasiri akamwambia: Ndoto inaashiria kwamba kweli utazaa mtoto mzuri. Lakini jihadhari naye asije akapigwa kijicho.


13 comments:

  1. Baraka Allah Allah akuzidishie elimu inshallah.

    ReplyDelete
  2. Asalam alaykum mimi mwanzo nilipo olewa nilikua naota napigana na wanawake ambao walinambia huyo mwanaume tutamchukua tuila baada ya kupata mtoto ndoto zangu zimekua zikibadilika na namuota mume wangu anamwanamke naomba tafsiri

    ReplyDelete
  3. SHUKRAN DOCTOR ALLAH AKUZIDISHIE MILANGO YA ELIMU

    ReplyDelete
  4. Asalaam aleikum...leo ni siku ya pili naota ndoto nikiwa na maiti..moja ni marehemu babu yangu akiwa ni mziwa wa afya na pili ni mjomba wangu aliye hai lakin nikimsaidia kutatua tatizo lake la mtu kutaka kumtapeli ila akiwa amezungukwa na badhi ya watu ambao wameshakufa na mwisho wa ndoto ya pili ni kuwa baada ya kubaini utapeli huo nilivunja kiti na kumnyooshea yule mtoto wa tapeli ambaye ni binti yupo na mwanae ambae alikuwa anamfunda maneno ya kuongea ili kutengeneza ushahidi mzuri wa kufanya huo utapeli nikachukua kipandw cha kiti kile nilichokivunja na kumuonyeshae yule mtoto na yule mtoto akavua viatu na kuondoka zake pamoja na mama yake.

    ReplyDelete
  5. Asalaam alleukum. Leo nimeota nimepata watoto mapacha kutoka kwa mwanamke ambaye sjmjui yaani nimezaa na binti ambaye simjui na sikuwa na habari Za ujauzito wake. Laini nimewapokea vizuri na kuwapenda wanangu. Imenibidi nimpe taarifa mama yangu ambaye amedurahia habari hiyo lakini mama yangu tayari amekwishatangulia mbele Za haki.ameonekana kufurahishwa na habari hiyo na nilivyomuuliza yule mwanamke niliyezaa naye hao mapacha akaniambia mama yangu alishajua kitambo tu sema alisubiri nimwambie. Hii ndoto imenipa tabu sana hadi nitake msaada wa tafsiri yake tafadhali.

    ReplyDelete
  6. Asalaam alleikum. Leo nimeota nimepata watoto mapacha kutoka kwa mwanamke ambaye sjmjui yaani nimezaa na binti ambaye simjui na sikuwa na habari Za ujauzito wake. Lakini nilivyopewa habari Za watoto hao nimejawa na furaha Kweli. Kuasi imebidi nikamueleze mama yangu ambaye tayari amekwisha tangulia mbele Za haki. Yeye binafsi kaonesha kufurahishwa na jambo hilo. Nilipomuuliza huyo binti niliyezaa naye akaniambia mama yangu alishajua kitambo tu sema alisubiri nimwambie mwenyewe. Ndito hii imenipa wasiwasi sana hadi mitake kujua nini maana yake tafadhali naomba msaada

    ReplyDelete
  7. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  8. mjamzito nimeota nimepata kazi nzuri serekalini ya jeshi mkubwa akaniuliza kuna kazi 2 moja ya security na nyengne ya office nikaamuulza ipi yenye mshahara mzuri akanejebu kuwa securitty mshahara wake mzuri rial800 na office rial 500 nikamwambia nataka securitty akasema mazali wewe mja mzito bora uwe office tutakupa mshahara huo juo rial800 nikafurahi nikakubali nikapelekwa office yangu kuanza kazi nikawa nafuraha ya kupata kazi nikamuona rafiki yangu kaja na yye kupata kaz akapa time ya break nikenda juu chumbani nikamuona bibi yangu amelala akashtuka kuamka akaniulza saangapi sahizi nikamjibu bado harusi nimekuja kutia poda nekamuhadithia kuwa mepata kazi na nikitoka kazini nitakupitia twende pamoja na mngr anataka kuja na sisi tutamchukua akasema sawa nikachuka kuendelea na kazi zangu ndipo nikaamka

    ReplyDelete
  9. me mja mzzito niko nabiashara yangu nimeota nimemalza kazi zangu nikafunga duka nikenda duka lengine kununua kitu nachohitajia nilipomaliza kununua nikatoka nikapita dukani kwangu nikaona duka lipo wazi geti la nje na taa zko wazi kuingia nikaiona kuwa silver fedha zote hakuna hata 1 zemechukulia vimebakishwa vitu vyengine bavo vya kawaida tu lakini vitu vya dhamani vyote vimebebwa nikatoka nje nikaona wahindi wanachukuaxmizigo kiwenda ndani ya duka lao mabegi ila sukuwaendea kwanza nikawauliza maduka yakokua majirani kwangu moja wote wamesema hawajui moja wapo akasema kuwa ameona ahindi wamefungua nakutoa vitu ndani nikamuliza inawajua akasema siwajui lakini hawa wahindi wahapa hapa mitaani ndio waloingia dukan kwako mana wamezoea kuiba nikawaendea wale wahindi walokua wanaweka mizigo yao ndani wamemaliza kutia mizigo yao ndani ya duka lao teary ila nikawaendea ndani na kuwambia wafungue mizigo yao waloleta wamekataa nikawambia kuwa kama hajafungua nakuleteeni police moja wapo anasema neno chafu nikamwambia nitakupiga usiniletee upumbavu mumenibia alafu unaleta ujinga wako kikamvuta sikio na kupga kibao akanyamaza ila me nimendelea kuwambia wafungue mizigo wanakataa nikatoka kwenda dukan kwangu kupga sim police nikaamkaa nini maana ya ndo hizi nilokutumia

    ReplyDelete
  10. Assalam alykum
    Dr mie naotaga nyoka wengi lkn kunaanaye nifukuzia na nikiwa mbio sana mpk namshinda au nasaidiwa na mtu mwingine naomba tafsiri hii tafadhali

    ReplyDelete
  11. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  12. Assalamu'alaykum..mimi ni mjamzito mara mbili nimeota nimezaa waroto pacha lkn hospitali mwisho nilipiga ultrusound nina miezi mitano yaani wiki 20 nikaambiwa nina mtoto mmoja..nini tafsiri ya ndoto hii sheykh?

    ReplyDelete
  13. Assalamu'alaykum..mimi ni mjamzito mara mbili nimeota nimezaa waroto pacha lkn hospitali mwisho nilipiga ultrusound nina miezi mitano yaani wiki 20 nikaambiwa nina mtoto mmoja..nini tafsiri ya ndoto hii sheykh?

    ReplyDelete